Tuesday, February 28, 2012

Mtetea aina ya Rhode Island red chotara


Mtetea aina ya Rhode Island red chotara wanatoa mayai makubwa ukilinganisha na kuku wengine. Wakubwa kwa uzito pia.

Mtetea aina ya Malawi

Mtetea aina ya Malawi huwa wana sifa kwa utagaji wa muda mrefu ukilinganisha na kuku wengine.

Maeneo ya mapumziko

Baada ya kazi ngumu ya kujituma katika kujenga taifa letu ni muhimu sana Mjasiliamali kukumbuka kunatakiwa kuwa na wakati wa mapumziko kwa ajili ya afya yako.
Tembelea maeneo haya huko Znz kupata hali ya hewa laini kwa ubongo wako.

Vifaranga aina ya Kuchi Chotara

Vifaranga aina ta Kuchi Chotara wanastahili mazingira magumu. Majogoo ni makorofi hivyo hutumika kwenye maonyesho ya kuku. Wanaonekana wembamba lakini ni wazito zaidi ya kuku aina ya Malawi

Kuku aina ya Rhode island red

Jogoo akipanda kuku mwingine yeyote kifaranga kinachotoka ni cha Rhode Island red original. Hawa ni kuku wenye uzito hata mpaka kilo 6 akilishwa vizuri kuanzia umri wa miezi mitatu hadi atakapouzwa ambapo anakua na umri wa miezi minne

Jogoo aina ya Malawi

Majogoo aina ya Malawi huonekana na Umbo kubwa hii ni kutokana na wingi wa manyoya lakini sio wazito sana kama majogoo wa aina nyingine. Lakini mitetea ikipata mbegu hii vifaranga wanakua na asili ya jogoo zaidi. Majogoo haya yanapatikana kwa ajili ya kuuzwa

Banda la kuku la Kisasa


Banda la Kisasa la kuwekea kuku wa wiki nne hadi mitetea na majogoo.
Banda hili linarahisisha sana ktk kuwatunza kuku wako kwa urahisi bila ya kusumbuliwa na magonjwa yanayotokana na kinyesi chao wenyewe kwani hawawezi kukikanyaga badala yake kinaangukia kwa chini na wao wakiwa wanasimamia juu ya nyaya laini ndogondogo.

Monday, February 27, 2012

Uzalishaji wa Kuku

Ujumbe huu nimegundua ni muhimu sana kwa wafugaji wa kuku kuufahamu.

Uzalishaji wa kuku,

Jinsi siku zinavyosogea mbele ndivyo hivyo utaalamu wa uzalishaji wa kuku unavyozidi kuendelea. Wafugaji wengi wa kuku binafsi au makampuni duniani, ambayo yanayo mashamba makubwa, na wanazalisha kuku wa biashara, waenaendelea kuzalisha kuku wa aina mbalimbali kwa madhumuni ya utagaji sana wa mayai au utoaji wa nyama bora. Kuku hawa hupewa majina mbalimbali na mara nyingi hutangazwa kwenye magazeti ili wafugaji wapate kununua. Kuku hawa wanazidi kuingia nchini Tanzania, kwa mfano Anak, Chunky na Cobb ambao ni wa nyama. Shaver 288 na Shaver 577 ambao ni wa mayai.

Kuku maalum wa nyama au mayai kama hawa wasitumike tena kwa kuendelea kuzalisha au kuchanganya na kuku wa kienyeji. Iwapo mfugaji atawatumia kuku hawa maalum kwa kuendelea kuzalishia au kuchanganya na kuku wa kienyeji kwa vizazi vya mbele, vizazi hivyo hudhoofika na kumletea mfugaji matatizo mengi kama magonjwa na mengineo. Kuku ambao wanafaa kuendelea kuzalishia au kuchanganya na kuku wa kienyeji ni wale ambao wenye damu halisi ya aina yake kwa mfano New Hampshire Red, Light Sussex na Rhode Island Red.Source from Wikipedia.

AINA ZA KUKU WA KIENYEJI

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI
Ndege wa kufuga ni kama vile kuku, bata, batamzinga, kanga na bata bukini. Kuku hasa ndio wanaofugwa zaidi na wanapatikana kwa urahisi.

Kuku wapo wa aina nyingi sana duniani. Kwa sasa tunafuga kuku wa kienyeji aina ya;
1. Malawi original
2. Malawi na mchanganyiko wa Mbeya na Singida
3. Rhode Island Red original
4. Rhode Island Red chotara
5. Rhode Island Red na bridi ya Australia
6. Barreck Rock
7. Kuchi Chotara
8. Light Sussex