Monday, February 27, 2012

Uzalishaji wa Kuku

Ujumbe huu nimegundua ni muhimu sana kwa wafugaji wa kuku kuufahamu.

Uzalishaji wa kuku,

Jinsi siku zinavyosogea mbele ndivyo hivyo utaalamu wa uzalishaji wa kuku unavyozidi kuendelea. Wafugaji wengi wa kuku binafsi au makampuni duniani, ambayo yanayo mashamba makubwa, na wanazalisha kuku wa biashara, waenaendelea kuzalisha kuku wa aina mbalimbali kwa madhumuni ya utagaji sana wa mayai au utoaji wa nyama bora. Kuku hawa hupewa majina mbalimbali na mara nyingi hutangazwa kwenye magazeti ili wafugaji wapate kununua. Kuku hawa wanazidi kuingia nchini Tanzania, kwa mfano Anak, Chunky na Cobb ambao ni wa nyama. Shaver 288 na Shaver 577 ambao ni wa mayai.

Kuku maalum wa nyama au mayai kama hawa wasitumike tena kwa kuendelea kuzalisha au kuchanganya na kuku wa kienyeji. Iwapo mfugaji atawatumia kuku hawa maalum kwa kuendelea kuzalishia au kuchanganya na kuku wa kienyeji kwa vizazi vya mbele, vizazi hivyo hudhoofika na kumletea mfugaji matatizo mengi kama magonjwa na mengineo. Kuku ambao wanafaa kuendelea kuzalishia au kuchanganya na kuku wa kienyeji ni wale ambao wenye damu halisi ya aina yake kwa mfano New Hampshire Red, Light Sussex na Rhode Island Red.Source from Wikipedia.

1 comment:

Agape Farms Tanzania Limited said...

Wadau;
Nimegundua ili kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji ambaye unaweza kukidhi mahitaji ya wateja wengi ni lazima uwe mbunifu wa kujitahidi kuwa na kila aina ya kuku iwezekanavyo ili uweze kutoa huduma ya uhakika.