Monday, October 13, 2014

Ujasiliamali na Lengo

Ujasiliamali ni kujituma na kuangalia mbele lile lengo ulilokuwa nalo kwenye moyo wako kujiona unafika wapi.... Malengo katika biashara ni kitu muhimu sana.

Thursday, May 17, 2012

A Chicken Egg Hatching A Baby Chick


Baby Chick,  it's good to know where the chicks comes from.

Give your mouth a taste

     

An egg must be the ultimate pre packed food and one of the first..So many ways to cook them and so cheap and filling.I often   wonder when man or woman  started realising they could cook an egg. Did they drop and break an  egg on a hot piece of ground and it started cooking? I am sure it must have been before humans  discovered a frying pan !

An egg is also a very good source of protein and unless you are a vegan very suitable for vegetarians.



Eggy bread is also called French bread and can be savoury or sweet. Kids love this. So quick and easy to with many variations. When I was young my mum used to make this and then dip it sugar and cinnamen .

Ingredients
  • 4 slices white or wholemeal  bread .
  • 2 eggs beaten with a little milk.
  • oil .
  • salt and pepper.
Method
  1. Beat the eggs with a little milk and add seasoning of salt and pepper.
  2. Heat a small coating of oil in a shallow frying pan
  3. dip bread in the egg mixture on both siodes and add to the pan cook on both sides until golden brown.
  4. You can make a sandwich first of ham or cheese and then dip…Yummy.
  5. For a sweet one you could have jam , honey or even fruit.

Friday, April 13, 2012

Bata mzinga Jike

Bata Mzinga Jike huyu kwa kiumbo huwa ni mdogo kiasi lakini anatoa mayai mengi na mazuri na pia nyama yake huwa ni laini ukilinganisha na bata mzinga dume.

Bata Mzinga dume (Turkey)

Ndege huyu hufahamika sana na wazungu wa nchi tajiri kwani ndio wengi wao chakula kikuu siku za sikukuu, wanapatikana nasi, ni bata watamu sana kwa nyama na mayai pia yanapatikana. Huyu ni bata aina ya mzinga na ni dume. Kula nyama ya bata kwa afya bora.

Friday, March 30, 2012

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI

Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi na afya bora katika familia
Kuku huleta faida kwa jamii .
Ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.

Faida;· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini     kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.


Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama) Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.

Hesabu rahisi za ufugaji wa kuku wa kienyeji;Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo, huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa nafaka. Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku. Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.

Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo
Source from Jamii forum.

Mtetea na Vifaranga wake - Tulipoanza mradi

Mtetea na vifaranga wake tuliendelea kujifunza kutoka kwa kuku wetu pale tulipokua tumeanza na mtetea huyu kwa kupata vifaranga 15 na wengine walikufa na kubakia 10 hata sasa wanakua na wenyewe kuwa mitetea na vijogoo, utajifunza kitu hapo kwani wanapokaa nje kwenye banda lao wakati wanawatamia baada ya kuaguliwa tunawachukua na kuwapeleka ndani kwenye joto zaidi ili kukua kwa uangalizi wa karibu

Kuku wa kienyeji wakitamia - Tulipoanza mradi

Kuku wa kienyeji wakitamia wakati tumeanza mradi tuliwaachia watamie kwa muda ili tuendelee kujifunza kutoka kwao kwa kuwa tlijua ni heri kwetu kujifunza zaidi kabla ya kuamua kuingia ktk mradi mzima.
wenyewe wakiwa wanatamia hawapendi kuingiliwa ingiliwa na mwanadamu na hata wenyewe kwa wenyewe ndio maana utaona tumewatenganishia kwa vibao kila mmoja asimuone mwenzie lakini wanawekewa chakula chao na maji.

Mabanda ya kuku - Tulipoanza mradi

Mabanda ya kuku hapo tulipoanza mradi huu, ninapenda sana kukuonyesha pale tulipotoka kwani kila lenye lengo dogo zuri linazaa lengo kubwa, utaweza kuona tulipoanza mradi huu tulianza na vibanda hivi vidogo na baada ya hapo tukaongeza hilo la katikati tukijitahidi kupawa joto pia wakati wa usiku na kuku wakipata eneo la kucheza kwa kiazi nje.
Neti hizo hapo juu ni kwa ajili ya kuzuia ndege waharibifu wa mifugo hapo kama kunguru, mwewe na wengineo.

Chakula cha kuku kwa kilo - Tulipoanza mradi

Chakula cha kuku tilipoanza mradi hapo mwanzoni mwanzoni, hakika kila kitu kikubwa kilianza kidogo kwanza. Ndivyo inavyoonyesha hapo tulipoanza kununua kwa kilo chakula cha kuku ambao hata na wenyewe walikua ni wachache wakati huo, tulianza kwa nunua kilo moja kwa shilingi elfu nne.