Friday, March 30, 2012

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI

Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi na afya bora katika familia
Kuku huleta faida kwa jamii .
Ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.

Faida;· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini     kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.


Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama) Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.

Hesabu rahisi za ufugaji wa kuku wa kienyeji;Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo, huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa nafaka. Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku. Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.

Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo
Source from Jamii forum.

No comments: