Tuesday, March 13, 2012

Ubora wa Yai la kuku wa kienyeji

Tofauti kati ya YAI LA KUKU WA KIENYEJI
na la kuku wa kisasa

Vi r u t u b i s h i vinavyopatikana kwenye yai la
kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya
chuma na virutubishi vya aina nyingine,
ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai
la kuku wa kisasa. Tatizo linaweza
kutokea pale ambapo wafugaji wa
kuku wa kisasa hawafuati taratibu
za ufugaji na pengine hawawapi
kuku vyakula muhimu
wanavyohitaji, hivyo wakati
mwingine kiini cha yai la kuku wa
kisasa huonekana kupungua rangi ya
njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.
Ninakushauri kula yai la kuku wa kienyeji lisilo
na madawa mengi na waliolishwa vyakula vya
kawaida kama hata mbogamboga yaani mchicha
spinachi na hata matembele.

Ulaji wa Yai bichi unamadhara ya vijidudu viitwavyo
kwa kitaalamu “SALMONELLA” vinavyoweza
kusababisha tumbo kuuma, kichefuchefu na
pia kuharisha. Vijidudu ya “Salmonella”
vinaweza kusababisha madhara makubwa
kwa watoto, wazee na wale wenye hali dhaifu
ya kimwili. Inashauriwa kupika yai mpaka liive kabisa,
na kuhakikisha kwamba hakuna ute unaoteleza.
Kama ni yai la kuchemsha, lichemshwe kwa
dakika kumi zaidi baada ya maji kuchemka.
Pia ni muhimu kuhakikisha kwamba vyombo vilivyotumika
Kuna nyama za aina mbili

Nyama nyeupe na nyama nyekundu. Nyama nyeupe
ni pamoja na samaki, KUKU, ndege wa aina
zote, bata, wadudu; na nyama nyekundu ni
pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo,
nguruwe na wanyama wa porini.
k u k o rogea yai bichi vinaoshwa kwa maji na
sabuni kabla ya kuvitumia tena kwa matumizi
mengine ili kuepuka maradhi.

No comments: