Tuesday, March 13, 2012

Chakula bora

Jamii ya kunde na vyakula vyenye
asili (Protini)
Husaidia kujenga mwili, kuboresha kinga na
kurudisha sehemu zilizochakaa,
Vyakula hivi ni kama maharagwe, njegere,
kunde, karanga, mbaazi, dengu, njugu,
samaki, KUKU, maziwa, jibini, dagaa,
mayai, maini, figo n.k.

Nafaka, mizizi na aina za ndizi
(carbohydrates)
Husaidia kuupa mwili nguvu na joto
Vyakula hivi ni mahindi, mchele, mtama,
ugugu, uwele, sandala, ulezi, ngano, viazi
vikuu na vitamu, magimbi, ndizi na mihogo.


Matunda na mboga za majani
(vitamini na madini)
Kundi hili hulinda mwili usishambuliwe na
magonjwa mbalimbali, huupa mwili vitamini
na madini. Vyakula hivi ni mboga zenya rangi ya kijani
kama mchicha, spinachi, majani ya kunde,
mhilile, mzimwe, majani ya maboga na
mrenda mbichi na bamia
Pia matunda, kwa mfano machungwa,
zabibu, fulu, ngweru, sada, ukwaju,
zambarau, karoti, mapapai, maembe na mapera.

No comments: